ZOLA FLEX ni MTAMBO JANJA WA NISHATI wa kwanza wa “Funga & Tumia” ambao unakuwezesha kutumia na kuchaji vifaa vyako muhimu bila jitihada nyingi wakati umeme wa gridi ya taifa unapokatika. ZOLA FLEX inafanya hivyo kwa kuhifadhi nishati ya jua iliyozalishwa, umeme wa gridi ya taifa na nishati iliyozalishwa kutoka kwenye jenereta katika betri zake imara na madhubuti za lithiamu-ion zinazofahamika kama Boksi la Nishati la FLEX.

Nishati iliyohifadhiwa inajazwa kupitia moja kati ya vyanzo vitatu – jua, umeme wa gridi ya taifa au jenereta – Kipaumbele ikiwa ni nishati ya jua kwani inapatikana bure isipokuwa wakati wa usiku ambapo huwa haipatikani.Nishati hii iliyohifadhiwa itatumika kuwezesha utumiaji wa vifaa utakavyotaka. Nishati iliyohifadhiwa katika Boksi inaweza kudumu usiku kucha kutegemeana na kiwango cha nishati kinachotumika na muda wa kutumika kwa vifaa.