Wateja wetu

TUMEWEZESHA UPATIKANAJI WA UMEME WA JUA KWA WATU MILIONI 1

Bara la Afrika linaongoza mabadiliko ya kidunia kwenye nishati endelevu kupitia nishati mbadala. Mitambo ya umeme wa jua ya ZOLA sasa inawezesha familia na biashara kote Afrika na popote duniani kuzalisha, kuhifadhi na kutumia nishati endelevu.

Uwezo wa kiuchumi wa biashara na jamii kote duniani utawaletea upatikanaji wa nishati safi ya jua na ya kuaminika saa 24 ambayo teknolojia ya ZOLA inahakikisha hilo linafanyika. Uchumi sio kitu pekee kinachofaidika na hilo, upatikanaji wa umeme kimsingi unaboresha afya, elimu, usawa wa upatikanaji wa huduma za kifedha, uwezeshaji wa wanawake na matokeo ya kimazingira kwa wale walionao.

Elimu

Utumiaji wa intaneti na rasilimali za elimu zinazopatikana mtandaoni hautawezekana bila kuwa na umeme. Simu ya mkononi iliyojaa chaji na utumiaji wa televisheni ni muhimu kukuza udadisi na mawasiliano ya kijamii. Taa za kuaminika zinaleta usalama, ulinzi na masaa mengi zaidi ya uzalishaji wakati wa jioni. ZOLA inajivunia kushirikiana na Shule ya Sekondari Wasichana ya Arusha Girls iliyopo Tanzania ambako mitambo ya umeme wa jua ya ZOLA inasaidia kupanua wigo wa fursa za elimu.

Afya

Kulingana na taarifa kutoka shirika la International Energy Agency, nchi zinazoendelea zinachangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa hali ya hewa, jambo ambalo linapelekea vifo vya watoto wanaozaliwa kabla ya muda stahiki kwa wastani wa vifo milioni 6.5 kila mwaka.

Upokeaji mkubwa wa usambazaji wa mitambo ya umeme wa jua ni muhimu sana.

Women Empowerment

Upatikanaji wa nishati kwa kiasi kikubwa utaboresha ustawi, hali ya kifedha na kijamii kwa wanawake. Intaneti, mawasiliano ya simu za mkononi na televisheni vina mchango mkubwa kuwawezesha wanawake kufahamu desturi mpya za kijamii na kupata taarifa. Nishati ya kuaminika inaweza kusaidia wajasiriamali wa kike kujenga biashara zao, kupata kipato, na kuwa na uhuru wa kifedha na kujitawala. Upatikanaji wa umeme kwenye hosipitali na vituo vya afya ni muhimu sana kwa afya ya wanawake na familia

Biashara ndogo

Intaneti, mawasiliano ya simu za mkononi, umeme kwa ajili ya matumizi ya compyuta mpakato (laptop), mashine, vifaa, taa na burudani ni muhimu kwa kila biashara. Nishati safi ya jua, nafuu na ya kuaminika inasaidia biashara kuweza kuhudumia wateja wengi zaidi, kuongeza masaa ya kufanya kazi, kujenga chapa yao na kupanuka katika kutoa huduma mpya na kupata fursa za kuzalisha kipato.

Makazi na Familia

Mitambo ya ZOLA inapatikana kupitia mfumo wa kulipia-kadiri-ya-matumizi. Wateja wanalipa malipo ya awali kisha ZOLA inafunga mtambo na fedha iliyobaki inalipwa kwa awamu kati ya miaka 2 hadi 3. Wateja wanaweza kumalizia gharama za malipo ya mtambo kwa matumizi yao ya sasa ya umeme wa jua kisha kuendelea kupata umeme wa jua bure na hivyo inawapunguza gharama za upatikanaji wa umeme kwao.

Uzalishaji

Kila kaya mpya inayotumia mitambo ya ZOLA inazuia kg 140 za kaboni dioksaidi na kg 1.45 za kaboni nyeusi kusambaa angani kila mwaka. Majenereta ya diseli kwa Nigeria peke yake yanazalisha hadi tani za metriki milioni 29 za CO2 kila mwaka ambazo ni sawa na wastani wa magari ya wasafairi milioni 6.3.

Tazama video fupi ya bidhaa yetu