Wasifu

UMEME POPOTE
MASAA 24

SAFARI YETU ILIANZA MWAKA 2011

Wazo halikuwa kuunda teknolojia kwanza, bali kuelewa kwanza mahitaji ya wateja na kile wanachoweza kumudu.

Kutoka kwenye ufahamu huo, timu ikaweza kuunda teknolojia sahihi inayoendana na mahitaji ya wateja.

JINSI TULIVYOANZA

Chanzo cha ZOLA Electric kilianzia kwenye safari aliyosafiri mwanzilishi mkuu Xavier Helgesen mwaka 2007 nchini Malawi. Alifikia kwenye kijiji cha uvuvi ufukoni mwa Ziwa Malawi ambako alialikwa kwa chakula cha jioni kwenye nyumba ya familia moja ambayo ni wenyeji hapo.

Alijifunza kuwa mwenyeji wake anategemea mafuta ya taa ambayo si salama ili kupata mwanga nyumbani kwake. Akajiuliza, kwanini kati ya watu aliokutana nao hakukuwa na yeyote aliyekuwa na angalau mtambo mdogo wa umeme wa jua? Je, ni changamoto ya teknolojia au ni shida nyingine?

Miaka Mitano baadae, ZOLA Electric ilianzishwa rasmi ikifahamika kama Off-Grid Electric . Waanzilishi walikuja Tanzania mwaka 2012 baada ya kufanyia kazi wazo hilo kwa mwaka mmoja katika chuo kikuu cha Oxford na kukusanya pesa kwa ajili ya uanzilishi. Walianzisha kampuni na ikaitwa Off Grid Electric.

Dhana haikuwa kujenga teknolojia kwanza bali kuelewa mahitaji ya wateja na gharama watakazoweza kuzimudu. Kwa kufahamu mambo hayo, wangeweza kutengeneza teknolojia ambayo inaendana na uhitaji wa wateja.

Leo, ZOLA ni kampuni ya nishati ya jua inayoongoza katika masoko inayoyahudumia ikiwa inatoa huduma kamili ya nishati jua ambayo inaweza kukidhi mahitaji yoyote ya nishati.

ZOLA Electric imeunda muundo wa kipekee na falsafa ya uhandisi kutokana na uelewa mkubwa tuliopata katika kuwahudumia wateja zaidi ya milioni 1. Wimbi la kwanza la nishati ya jua lilitia mkazo kwenye nchi zilizoendelea ambapo wateja hukabiliana na bili za matumizi yao kupitia mifumo mbalimbali. 

"Kama kuzalisha nishati yako binafsi ni rahisi na ni njia ya kuaminika zaidi ya kununua umeme kutoka kwenye gridi ya taifa, kwanini usifanye hivyo?"

Uongozi wa ZOLA ELECTRIC

Bill Lenihan

Chief Executive Officer

Partner @ Fremont Partners / Calera Capital, EVP International @ Switch Lighting, Goldman Sachs, Credit Suisse, MBA @ Wharton, BA @ UCLA

Doye Ogionwo

Chief Commercial Officer

CEO @ Triffant Resources, Group CCO @ Helios Towers, Partner @ NEWE Partners, MBA @ Carnegie Mellon

Martijn Bouwmeester

Chief Financial Officer

Finance Director @ Johnson & Johnson Msc. Industrial Engineering & Mgmt, Twente University

Sau Ngosi

Chief Technology Officer

CTO @ Schneider Electric, Board Member @ Warm Heart of Africa Foundation, P.Eng @APEGBC., B.Eng

Steven Van Maasakker

General Council

Executive Director Global Legal Affairs - General Counsel @ Heineken

Robert Falcon

VP Manufacturing and Supply chain

Global Director Human Capital - Nicola Douglas

Nicola Douglas

Global Director - Human Capital

15+ years Human Resources experience in USA, Europe and Asia. SDA Bocconi School of Management (Italy) MBA and Fairfield University (US) Bachelor

Bodi ya wakurugenzi

Bill Lenihan

Director

Partner @ Fremont Partners / Calera Capital, EVP International @ Switch Lighting, Goldman Sachs, Credit Suisse, MBA @ Wharton, BA @ UCLA

Xavier Helgesen

Director

Skoll Scholar + MBA @ Oxford, Co-Founder @ Better World Books, Indaba Systems

Nancy Pfund

Director

Founder and Managing Partner of DBL Partners, JPMorgan, Hambrecht & Quist, MA @ Stanford, MBA @ Yale

Steve Hall

Director

Managing Director @ Vulcan Capital

Tope Lawani

Director

Co-founder and Managing Partner of Helios Investment Partners, TPG, MIT, Harvard Law, MBA @ Harvard

Lyndon Rive

Director

Co-founder @ SolarCity now Tesla Energy. Co-Founder @ Everdream, Board @ NatGeo, GivePower, World Spine Care. U.S. National Underwater Hockey Team member.

Mfululizo wa matukio

 • 2012 - ZOLA Ilianzisha kama "M-POWER"

  ZOLA ilianzishwa kama “M-Power” Arusha, Tanzania ambapo hadi mwishoni mwa 2012 ilipata wateja wake 1,000 wa kwanza.

 • 2014 - ZOLA Inafunguliwa Tanzania

  ZOLA ilipanuka kwa haraka kote Tanzania kutokana na wateja zaidi ya elfu 10 kuchagua kutumia bidhaa za ZOLA. Sambamba na hilo, ZOLA ikaingia ubia na International Finance Corporation katika mfuko wa dola za kimarekani milioni 7 ($7 Million facility) kwa ajili ya maeneo yasiyo na umeme wa gridi ya taifa ambao ulikuwa ni uwezeshwaji mwingine wa kwanza katika sekta hiyo.

 • 2015 - ZOLA inazindua mitambo ya M-series

  OLA ilipata mtaji katika harambee iliyoongozwa na washirika wa DBL. Nancy Pfund akajiunga na baraza la wakurugenzi. ZOLA ikazindua toleo lake la tatu la bidhaa zake ambapo uwezo wa nishati uliongezwa mara 10 zaidi ya matoleo yaliyopita.

 • 2016 - Ofisi zinafunguliwa Rwanda

  ZOLA pamoja na EDF Energy walitangaza ushirikiano wa kibiashara ili kupanua fursa za upatikanaji wa nishati Afrika magharibi ambapo walianza utendaji kazi Côte d'Ivoire.

 • 2017 - mtambo wa ZOLA FLEX unazinduliwa

  ZOLA begins operations in Nigeria, Africa's biggest market. Nigeria has more diesel generators than households. Unlike its approach in other markets, ZOLA's target is not only off-grid households but also those that are connected to an unreliable grid that demands the use of dirty, dangerous and unhealthy diesel generators.

 • 2018 - ZOLA inafungua tawi Nigeria

  Nigeria ina idadi kubwa ya majenereta ya diseli kuliko idadi ya kaya. Lengo la ZOLA sio kufikia kaya zilizopo kwenye maeneo yasiyo na umeme wa gridi ya taifa peke yake bali pia kufikia kaya ambazo zimeunganishwa na umeme wa gridi ya taifa usio wa uhakika hivyo kulazimu matumizi ya majenereta ya diseli ambayo ni hatari na sio salama kwa afya.

 • 2019 - ZOLA INFINITY INAZINDULLIWA NIGERIA

  Bidhaa za ZOLA zinawezesha upatikanaji wa umeme wa jua kwa zaidi ya watumiaji milioni 1 kila siku. Kampuni ilizindua mitambo ya INFINITY ambayo inatoa umeme wa mkondo geu(AC) saa 24 popote ikiwa na betri ya lithiamu-ion, paneli ya jua na umeme wa gridi ya taifa kama nishati ya ziada unapokuwepo.

 • 2020 - Mradi wa gridi ya umeme wa sola, Rwanda

  Mradi wa 120 kWp Gakagati sasa unawezesha upatikanaji wa umeme kwenye makazi 931, biashara 58, vituo vya dini 3, shule 1, kituo cha afya na mitambo 5 ya umwagiliaji ikiwa na matarajio ya kuongezeka kufikia 240kWp ndani ya miaka 2. Mitambo imara ya ZOLA ya INFINITY ndio msingi wa gridi ndogo ya umeme.

Tuzo

WASHIRIKA NA WADAU

Wawekezaji na washirika wa kibiashara wa ZOLA Electric ni pamoja na Tesla, General Electric, EDF Energy, DBL Ventures, Helios Investment Partners na Total.

Jisajili kwenye Jarida letu

Usikose habari zinazokuja kutoka ZOLA Electric, Jiunge sasa!