ZOLA Electric

ZOLA iliuundwa California na kuzaliwa Afrika ikiwa na ndoto ya kuwezesha upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa mtu yeyote mahali popote. Ilizaliwa kutokana na wazo lililozaliwa chuo kikuu cha Oxford 2012 lililokuwa na lengo la kutoa nishati kwa mabilioni ya watu wasiokuwa au wenye upatikanaji hafifu wa umeme wa gridi ya taifa. Wazo hili liliwezekana kutokana na uvumbuzi wa teknolojia kama teknolojia ya uvunaji bora wa nishati ya jua na uhifadhi, mfumo wa kulipia-kadiri-ya-matumizi(PayGo microfinance) na huduma za kifedha kupitia simu za mkononi. Ilizaliwa Afrika, ambapo tuliweza kujua tunahitaji nini ili kuweza kuunda mtambo wa kwanza wa nishati ya jua ambao uliwezesha upatikanaji wa nishati safi kwa wote. Kupitia teknolojia ya hali ya juu, imetengenezwa kuweza kudumu kwa muda mrefu na NASA imeidhinisha kituo cha uzalishaji Malaysia. 

Matamanio yetu ya kuwezesha upatikanaji wa nishati kote Afrika na mawazo ya kimaendeleo mapema yaliwavutia wawekezaji imara na baadhi ya wafanisi bora duniani wa teknolojia ya nishati safi. Safari hii ya kusisimua kuanzia kwenye kuundwa kwa dhana mpaka ukuaji imeona ZOLA ikipanua wigo wa bidhaa na huduma zake katika nchi zinazoendelea na kuwa na zaidi ya watumiaji wa kila siku milioni moja ndani ya miaka minne.Tunaaminika na watumiaji kwasababu ya kanununi yetu ya msingi ya kimaadili ya Wateja Kwanza na inaendelea kutupeleka mbele.

Zola Electric inavumbua mfumo wa uzalishaji na usambazaji wa nishati. Matoleo yetu mapya ya bidhaa yameleta sokoni teknolojia ya kisasa inayoongoza ya uzalishaji wa nishati kupitia paneli za jua na uhifadhi wa nishati hiyo katika betri. Kwa mara ya kwanza katika historia tumefanikiwa kutoa nishati ya jua ambayo ni safi, nafuu, na ya kuaminika pamoja na suluhisho dhabiti la uhifadhi wa nishati kwa matumizi ya nyumbani au kwenye biashara.

ZOLA Electric ni kampuni ya kimataifa, tuna ofisi kwenye nchi 10 katika mabara manne. Nguvukazi yetu imara ndio nguvu yetu ya msingi, inatupa uwezo wa ushindani dhidi ya masuluhisho mengine. Pamoja tunafanya kazi kuelekea katika lengo moja – kuangaza dunia na kudhihirisha uwezo wa mwanadamu. Kama kampuni yetu inavyoendelea kukua, kanuni za maadili ZOLA ni msingi unao tuunganisha pamoja:

  • Wateja kwanza – Tunawasikiliza, tunawaheshimu na kuwahudumia.
  • Wafanyakazi wetu ni bora – Tunathamini usalama, heshima na uadilifu. Tunajenga viongozi wetu wa siku za baadaye.
  • Bidhaa zetu ni za kishujaa – Mitambo ya nishati iliyoundwa kwa ufanisi ambayo daima inakidhi matarajio ya wateja wetu. Daima tunajitahidi kuwafurahisha watumiaji wa bidhaa zetu.
  • Utendaji wetu ni urithi wetu – Tunafanya kazi ili kuwa kampuni yenye viwango vya kimataifa inayotoa teknolojia madhubuti ya nishati. Daima tunalenga kuwa na ubora wa hali ya juu.

Kanuni hizi nne za maadili zinaiunganisha Zola katika HALI YA KUWA PAMOJA, sisi ni TIMU MOJA , yenye  NDOTO MOJA.