FAQ

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu Bidhaa za ZOLA

Je, naweza kulipia pesa kidogo kidogo(pungufu na malipo ya mwezi) na kupewa tarakimu?

Ndio, unaweza kununua umeme wa siku moja au zaidi kabla ya muda ulionunua umeme mara ya mwisho. Kulingana na mkataba wako malipo ni kwa mwezi lakini unaweza kulipa malipo ya siku moja kila siku bila kukosa.

Sijapata tarakimu za umeme nilionunua mara ya mwisho.

Sogea karibu na mtambo wako au andaa kalamu na karatasi kisha PIGA BURE 0800 752 222 kama utapiga simu kupitia namba yako ya simu uliyosajiliwa nayo ZOLA, bonyeza 2 kisha bonyeza 1 tarakimu zako zitasomwa. Kama utapiga simu kupitia namba tofauti na uliyosajiliwa nayo ZOLA, bonyeza 2 kisha bonyeza 2 tena na kisha bonyeza 1 tarakimu zako zitasomwa.

Nimekamilisha malipo ya kumiliki mtambo lakini mtambo wangu haujafunguliwa (unahitaji tarakimu).

Ili kupata tarakimu ikiwa tayari umemiliki mtambo tafadhali wasiliana nasi kupitia moja ya njia zifuatazo:

 1. WhatsApp – 0746 844 013 
 2. Instagram – zolatanzania
 3. Facebook – ZOLA Tanzania
 4. Twitter – ZolaTanzania
Je, huduma za matengenezo ya mtambo nyumbani/kufungiwa mtambo mpya zinachukua muda gani kunifikia?

Huduma zetu zinazohusisha kutembelewa nyumbani ni ndani ya siku saba za kazi baada ya kufunguliwa taarifa au kufanya malipo kwa huduma zitakazohitaji kulipiwa.

Napata masaa machache ya mwanga katika mtambo wangu wa ZOLA.

Mitambo ya toleo la L-series ina uwezo wa kufanya kazi kwa kati ya masaa 3 – 6, toleo la M-series masaa 6 – 10 na toleo la Flex masaa 8 au zaidi kulingana na matumizi. Ili kupata mwanga kwa masaa zaidi, tafadhali fanya mambo yafuatayo:

 1. Safisha paneli yako angalau mara moja kwa wiki kwa kutumia maji safi na kitambaa laini, usitumie sabuni.
 2. Hakikisha paneli yako inapigwa na jua wakati wote na haijakingwa na miti au kivuli. 
 3. Zima taa zako wakati wa mchana na wakati wa usiku tumia mwanga hafifu endapo hakuna ulazima wa kutumia mwanga mkali au zima taa kwenye maeneo yasiyotumika. 
 4. Usitumie vifaa vingi wakati wa usiku. 
Mtambo wangu hauingizi moto.

Tafadhali fanya mambo yafuatayo:

 1. Safisha paneli yako angalau mara moja kwa wiki kwa kutumia maji safi na kitambaa laini, usitumie sabuni.
 2. Hakikisha paneli yako inapigwa na jua wakati wote na haijakingwa na miti au kivuli.
 3. Chunguza kama waya wa paneli umelegea au umeharibika.
 4. Zingatia hali ya hewa, kipindi cha mvua na mawingu kasi ya mtambo kupokea moto hupungua. 
Je, imebaki Tsh ngapi ili niweze kumiliki mtambo wangu wa ZOLA?

Ili kupata taarifa za malipo yako tafadhali wasiliana nasi kupitia moja ya njia zifuatazo:

 1. WhatsApp – 0746 844 013 
 2. Instagram – zolatanzania
 3. Facebook – ZOLA Tanzania
 4. Twitter – ZolaTanzania
Salio la umeme katika mtambo wangu linaisha lini?

Ili kufahamu salio katika mtambo wako linaisha lini tafadhali wasiliana nasi kupitia moja ya njia zifuatazo:

 1. WhatsApp – 0746 844 013 
 2. Instagram – zolatanzania
 3. Facebook – ZOLA Tanzania
 4. Twitter – ZolaTanzania
Je, naweza kubadilisha namba yangu ya simu niliyosajiliwa nayo ZOLA?

Ndio, unaweza kubadilisha namba ya simu uliyosajiliwa nayo ZOLA. Ili kufanikisha hilo tafadhali wasiliana nasi kupitia moja ya njia zifuatazo:

 1. WhatsApp – 0746 844 013 
 2. Instagram – zolatanzania
 3. Facebook – ZOLA Tanzania
 4. Twitter – ZolaTanzania
Nimefanya malipo kuja ZOLA lakini muamala haujakamilika (Tigopesa, M-pesa na Airtel money).

Tafadhali zingatia mambo yafuatayo; 

 1. Angalia kwenye simu yako kama umerudishiwa sms ya kuthibitishwa kwa muamala. 
 2. Angalia kama kiwango cha pesa ulichotuma kimetoka kwenye akaunti yako. 
 3. Zingatia maelekezo yote uliyokuwa unapatiwa na mtandao husika wakati ukifanya muamala mfano, “Samahani huna salio la kutosha”. 

Endapo pesa imetoka kwenye akaunti yako na umepokea sms ya uthibitisho wa muamala na haujapokea tarakimu zako tafadhali wasiliana nasi kupitia moja ya njia zifuatazo:

 1. WhatsApp – 0746 844 013 
 2. Instagram – zolatanzania
 3. Facebook – ZOLA Tanzania
 4. Twitter – ZolaTanzania
Je, mitambo na vifaa vya ZOLA vinauzwa Tsh ngapi?

Tafadhali zingatia mambo yafuatayo; 

 1. Angalia kwenye simu yako kama umerudishiwa sms ya kuthibitishwa kwa muamala. 
 2. Angalia kama kiwango cha pesa ulichotuma kimetoka kwenye akaunti yako. 
 3. Zingatia maelekezo yote uliyokuwa unapatiwa na mtandao husika wakati ukifanya muamala mfano, “Samahani huna salio la kutosha”. 
Je, naweza kupatiwa punguzo la bei ya mtambo wa ZOLA?

Kwa wateja wanaotumia mfumo wa malipo ya kidogo kidogo kwa miaka mitatu wanapatiwa punguzo la bei endapo wataweza kulipa zaidi ya kiwango cha malipo ya mwezi mara kwa mara.

Je, naweza kumiliki mtambo wangu wa ZOLA mapema zaidi ya miaka 3?

Ndio, unaweza kumiliki mtambo wako wa ZOLA mapema sana endapo utachagua kununua mtambo wako katika mfumo wa kulipa malipo yote papo hapo au wakati wowote utakapokamilisha kiwango cha malipo yanayohitajika ili kuweza kumiliki mtambo wako. 

Je, bidhaa za ZOLA zina warantii ya muda gani?

Sehemu ya msingi ya mtambo wa ZOLA (Boksi, paneli na taa) ina warantii ya miaka 5 dhidi ya ubovu kutoka kiwandani, vifaa vingine(TV, Chaja ya simu, Tochi, Rimoti ya Tv, Radio) vina warantii ya mwaka 1 dhidi ya ubovu kutoka kiwandani.

Je, ZOLA itanipatia TV nyingine bure endapo TV yangu itaibiwa?

Hapana, fidia ya TV hutolewa endapo Tv ya awali itadhihirika kuwa na ubovu kutoka kiwandani ndani ya mwaka 1 wa warantii.

Je, naweza kutumia vifaa visivyo vya ZOLA kama jokofu, pasi, subwoofer, Tv ya kampuni nyingine au incubetor kwenye mtambo wangu wa ZOLA?

Hairuhusiwi kutumia vifaa visivyo vya ZOLA kwenye mtambo wa ZOLA isipokuwa king’amuzi kwa wateja wenye mitambo yenye TV.  Matumizi ya vifaa visivyo vya ZOLA tofauti na king’amuzi husababisha uharibifu wa mtambo.    

Kwa wateja wanaotumia mtambo wa ZOLA FLEX POWER 1 wanaruhusiwa kutumia vifaa visivyo vya ZOLA vinavyotumia kiwango cha juu kabisa cha nishati kisichozidi 65W mfano kompyuta mpakato(laptop). Kutumia vifaa visivyo vya ZOLA vinavyotumia kiwango cha nishati zaidi ya 65W katika mtambo huu husababisha uharibifu wa mtambo.

Je, mtambo wa ZOLA unaweza kusababisha mlipuko wa moto?

Hapana, mitambo ya ZOLA imeundwa kwa muundo dhabiti ambao ni rafiki kwa mazingira na hauwezi kusababisha mlipuko wa moto.

Je, kitengo cha huduma kwa wateja ZOLA kinatoa huduma kwa wateja kwa muda gani?
 1. Kitengo cha huduma kwa wateja cha ZOLA kinatoa huduma kwa wateja masaa 24 siku zote saba za wiki(24/7)
Je, tarakimu za umeme zinaweza kuingia moja kwa moja kwenye mtambo wangu wa ZOLA bila kuingiza kwa mkono?

Kwa mitambo ya toleo la Flex, tarakimu za umeme zinaweza kuingia moja kwa moja kwenye mtambo kupitia mtandao, endapo eneo la mteja halina mtandao italazimu tarakimu kuingizwa kwenye mtambo kwa mkono. Kwa mitambo ya toleo la L-series na M-series inalazimu kuingiza tarakimu za umeme kwenye mtambo kwa mkono.

Je, naingizaje tarakimu kwenye mtambo wangu wa ZOLA?
 1. Kwa mitambo ya toleo la L-series, bonyeza alama ya mshale kisha bonyeza alama ya reli, ingiza tarakimu zako kisha malizia kwa kubonyeza alama ya mshale. 
 2. Kwa mitambo ya toleo la M-series, bonyeza alama ya nyota mara 2 kisha ingiza tarakimu zako na malizia kwa kubonyeza alama ya reli. 
 3. Kwa mitambo ya toleo la Flex angalia vitufe vitatu vilivyopo kwenye mtambo, bonyeza kitufe cha kwanza kushoto mara 2 kisha bonyeza kitufe cha katikati hadi itokee namba husika. Hamia kisanduku kinachofuata kwa kubonyeza kitufe cha kulia kisha bonyeza tena kitufe cha katikati ili kupata namba inayofuata kisha bonyeza kitufe cha kulia tena ili kuhamia kwenye kisanduku kinachofuata. Fanya hivyo mpaka ujaze tarakimu zote 12 kwenye visanduku kisha malizia kwa kubonyeza kitufe cha upande wa kulia.
Je, kitengo cha huduma kwa wateja ZOLA kinatoa huduma kwa wateja kwa muda gani?
 1. Kitengo cha huduma kwa wateja cha ZOLA kinatoa huduma kwa wateja masaa 24 siku zote saba za wiki(24/7)
Je, maduka ya ZOLA yanafanya kazi wikiendi?
 1. Maduka ya ZOLA yanatoa huduma siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 09:00am hadi 06:00pm na Jumamosi kuanzia 09:00am hadi 04:00pm.
Je, naruhusiwa kuondoka na mtambo wangu wa ZOLA kama nitahamia mahali pengine?
 1. Ndio, unaruhusiwa kuhama na mtambo wako kwa kuzingatia kuwa utaendelea kulipia mtambo kama bado haujakamilisha malipo. Kama utataka usaidizi wa muhudumu wetu kuja kuufungua mtambo ada ni Tsh 5000. Endapo utaweza kumudu zoezi la kuufungua mtambo hautotozwa ada yeyote na baada ya kufika katika eneo jipya utapaswa kutufahamisha mahali ulipohamia.
Je, nifuate hatua gani ili niweze kutuma pesa ZOLA kupitia M-pesa?
 1. Tafadhali fuata hatua zifuatazo:
  1. Piga *150*00# (Kisha tuma)
  2. Chagua 4 (Lipa kwa Mpesa)
  3. Chagua 3 (Chagua kwenye orodha)
  4. Chagua 9 Zaidi
  5. Chagua 4 (Nishati mbadala)
  6. Chagua 5 (Zola)
  7. Chagua 1 (Weka namba ya akaunti)
  8. Enter Account – andika namba ya mita yako ambyo imeandikwa ubavuni mwa mita yako (kisha tuma)
  9. Weka kiasi (weka kiasi cha salio unachotaka kununua)
  10. Weka namba ya siri ya M-pesa
  11. Bonyeza 1 kuthibitisha malipo
  12. Subiri dakika 30 ili kupata ujumbe wa ZOLA wenye tarakimu 16 au 12 za umeme.
Je, nifuate hatua gani ili niweze kutuma pesa ZOLA kupitia Airtel Money?
 1. Tafadhali fuata hatua zifuatazo:
  1. Piga*150*60#
  2. Chagua 5, “Lipia Bili”
  3. Chagua namba 4 “Chagua  kampuni”
  4. Weka namba ya biashara ( 240240 )
  5. Ingiza kiasi cha pesa
  6. Ingiza namba ya kumbukumbu
  7. Ingiza namba ya siri kulipia ZOLA
  8. Subiri dakika 30 ili kupata ujumbe wa ZOLA wenye tarakimu 16 au 12 za umeme.
Je, nifuate hatua gani ili niweze kutuma pesa ZOLA kupitia Tigopesa?
 1. Tafadhali fuata hatua zifuatazo:
  1. Piga *150*01# 
  2. Chagua 4 “Lipia bili” 
  3. Chagua 3 “Ingiza namba ya kampuni”  
  4. Weka namba ya kampuni “240240” 
  5. Ingiza namba ya Malipo(Namba ya Boksi/Mita)
  6. Ingiza kiasi cha pesa. 
  7. Ingiza namba ya siri
  8. Subiri dakika 30 ili kupata ujumbe wa ZOLA wenye tarakimu 16 au 12 za umeme.
Je, namba ya kampuni ya kufanyia malipo ni ipi?
 1. Namba ya kampuni ya kufanyia malipo kupitia huduma za kifedha kwa kutumia simu za mkononi ni 240240.
Je naweza kutuma pesa ZOLA kupitia HaloPesa?

Hapana, ZOLA bado haijawezesha mfumo wa kupokea malipo kupitia HaloPesa.

Je, naweza kukopeshwa tarakimu za umeme?

Hapana, ZOLA bado haijawezesha mfumo wa kukopesha wateja tarakimu za umeme.

Je, naweza kupandishwa daraja la huduma ili nipate mtambo mkubwa zaidi?

Hapana, kwa sasa ZOLA haina utaratibu wa wateja kupanda daraja la huduma. Wateja wanashauriwa kukamilisha malipo ya mtambo walionao, kisha kununua mtambo mkubwa zaidi.

Je, naweza kusitisha mkataba wangu na ZOLA?

Ndio, ZOLA inaruhusu wateja kusitisha mkataba wakati wowote.

Je, nitapatiwa zawadi gani endapo nitaunganisha wateja wapya na ZOLA?

ZOLA inajivunia kuwa na wateja wapya wengi wanaounganishwa na ZOLA kupitia wateja wa zamani hivyo inamzawadia Tsh 10,000 mteja wa zamani kwa kila mteja mmoja mpya atakayetuunganisha naye.

Huduma bora hadi nyumbani kwako
FAHAMU ZAIDI
Fahamu kituo cha mauzo kilichopo karibu nawe
TAFUTA
KWA MSAADA ZAIDI, PIGA BURE

0800 752 222