Washirika

WASHIRIKA WETU WA KIBIASHARA

DISTRIBUTED POWER AFRICA

Shirika la DPA linaongoza katika soko kwa uvumbuzi wa huduma za nishati ya jua. Tunafanya kazi Kenya, South Africa na Zimbabwe. Sehemu ya kundi la Econet ya makampuni, Distributed Power Africa (DPA) inawapatia wateja wafanyabiashara na wenye viwanda ufungaji madhubuti wa umeme wa jua bila kutanguliza malipo ya awali.

EQUATORIAL POWER

Shirika la Equatorial Power linaleta Timu imara pamoja na rekodi nzuri katika miradi ya nishati mbadala na uwezeshaji wa upatikanaji wa nishati. Shirika limeanzisha upatikanaji wa umeme katika maeneo yasiyo na umeme wa gridi ya taifa na limeendeleza huduma hiyo kupitia ubunifu wa mpango biashara imara uliotia mkazo kutatua upungufu wa thamani katika usindikaji wa mazao Afrika vijijini.

MICRO POWER

Mwanzilishi nchini Brazil, Shirika la Micropower limeleta dhana ya bSaaS, kutoka kwenye neno la Kiingereza battery-Storage-as-a-Service, hivyo kuleta mapinduzi katika soko la nishati nchini humo.