ZOLA Electric

MASWALI A MARA KWA MARA

Je, ZOLA ELECTRIC ni nini?

ZOLA ELECTRIC ni kampuni iliyoanzia Silicon Valley ambayo ilianzisha mfumo wa kulipia-kadiri-ya-matumizi ili kutoa nishati safi ya jua, nafuu na ya kuaminika kwa wakazi na wafanyabiashara katika maeneo yasiyo na yenye umeme wa gridi ya taifa pamoja na upatikanaji hafifu wa umeme huo. Mtambo wa ZOLA wa uzalishaji wa nishati ya jua na uhifadhi madhubuti ulioundwa California umewezesha upatikanaji huru wa nishati ili kila mtu, popote, aweze kuzalisha, kuhifadhi na kutumia nishati endelevu. Upatikanaji wa nishati kwenye nchi zinazoendelea unabadilika kwa kasi kubwa. Upokeaji mkubwa wa suluhisho la nishati la ZOLA katika maeneo mengi unamaanisha kwamba familia na biashara sasa zinaweza kupata nishati popote zilipo, bila kujalisha hali zao.

Je, ZOLA ELECTRIC inaendesha shughuli za kikazi wapi?

ZOLA ELECTRIC inatoa huduma Afrika Mashariki na Magharibi – Nigeria, Ghana, Côte d’Ivoire, Rwanda na Tanzania. Maabara ya ZOLA ELECTRIC ya utafiti na maendeleo ipo San Francisco, California, USA. Makao Makuu ya ZOLA yapo Amsterdam, Netherlands.

Je, ZOLA ELECTRIC ilianzishwaje?

Mwaka 2012 Erica Mackey, Joshua Pierce na Xavier Helgesen walikutana Chuo kikuu cha Oxford. Baada ya kuhitimu programu ya MBA ya Oxford, walianzisha ZOLA ELECTRIC ili kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa nishati katika nchi zinazoendelea kupitia muundo madhubuti na endelevu, uhandisi na shughuli za kibiashara. Uvumbuzi wa teknolojia ya ulipaji kama, mfumo wa kulipia-kadiri-ya-matumizi na huduma za kifedha kupitia simu za mkononi iliyoambatana na kushuka kwa gharama za paneli za jua na betri za lithiamu-ion ulifungua fursa za suluhisho la kisasa dhidi ya ukosefu wa nishati.

Timu iliishi na kufanya kazi Tanzania kwa miaka mingi ili kupata uelewa halisi wa mandhari ya nishati Afrika. Walifanyia kazi mambo waliyojifunza ili kutengeneza na kuwezesha upatikanaji wa mitambo ya nishati mbadala ya gharama nafuu ambayo itakidhi mahitaji mahsusi ya nishati kwa Waafrika.

Je, nani ni washiriki wa uwekezaji na ushauri wa ZOLA ELECTRIC?

ZOLA ELECTRIC inapata ushauri na uwekezaji kutoka kwenye Baraza lenye wawekezaji wakuu katika masuala ya nishati kama Tesla, General Electric, EDF Energy, DBL Ventures, Helios Investment Partners, Omidyar Network, Total, FMO entrepreneurial development bank, responsAbility, SunFunder and the U.S Agency for International Development. Fahamu zaidi kuhusu wawekezaji wa ZOLA ELECTRIC kupitia zolaelectric.com/about-us.

Je, leo ZOLA ELECTRIC inatoa nishati safi kwa watu wangapi?

ZOLA ELECTRIC imefunga zaidi ya paneli za jua 200,000 + mitambo madhubuti wa uhifadhi wa nishati na inahudumia zaidi ya watumiaji milioni 1 duniani kila siku.