ZOLA Electric

Katika karne ijayo, sekta ya nishati mbadala itakuwa moja ya waajiri wakubwa duniani. ZOLA ELECTRIC inaongoza harakati za kuandaa siku bora zijazo kwa kila mtu na kila mahali.

Tumeajiri zaidi ya wafanyakazi 2,000 na tunatengeneza nafasi mpya za kazi kila mwezi. ZOLA ELECTRIC imejikita kukuza uwezo wa jamii ya ndani ya maeneo tunayotoa huduma. Kama sehemu ya lengo hilo, tunakuza fursa za upatikanaji wa ujuzi na kuendeleza uwezo wa wafanyakazi wote. ZOLA inatambuliwa kama moja ya sehemu nzuri ya kuajiriwa Afrika.

Tunatoa fursa za kiuchumi kwa wafanyakazi wenye shauku na uwezo mkubwa kiutendaji ambao wanatamani kuchangia kwenye mazingira ya uanzilishi wenye kasi kubwa. Tumejikita kuongeza thamani katika jamii za ndani ya maeneo tunayotoa huduma na kutengeneza njia za wafanyakazi wetu hodari wenye umri mdogo kukua na kuweza kushika nafasi za umeneja na uongozi.

LinkedIn

Nafasi mpya za kazi